Kolonia Santita
Author | : Enock Maregesi |
Publisher | : AuthorHouse |
Total Pages | : 407 |
Release | : 2012-09-17 |
ISBN-10 | : 9781477222973 |
ISBN-13 | : 1477222979 |
Rating | : 4/5 (73 Downloads) |
Download or read book Kolonia Santita written by Enock Maregesi and published by AuthorHouse. This book was released on 2012-09-17 with total page 407 pages. Available in PDF, EPUB and Kindle. Book excerpt: 'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi' ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya iliyoandikwa na Enock Abiud Maregesi. Inazungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC) au Tume ya Dunia; na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighafi ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya – na kung’oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifi a ya Magharibi – na duniani kwa jumla. Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa Watanzania, Wakenya na Waganda – na jamii nzima ya Afrika ya Mashariki inayozungumza Kiswahili – na walowezi wa jamii yote ya Kiswahili duniani.